Binti mmoja alikuwa akiendesha gari akiwa na baba yake. Wakiwa njiani ghafla mvua kubwa ikaanza kunyesha na kuleta tufani, yule binti akamuuliza baba yake, "Nifanyeje?" Baba yake akamwambia "endelea kuendesha".. Magari yakaanza kusimama na kuegesha pembeni kwa kuhofia tufani ambayo ilikuwa kubwa mno. "Nifanyeje?." Binti akamuuliza baba yake?
"Endelea kuendesha," baba yake akajibu.
Mbele yake tena akaona malori makubwa kabisa yakiegesha pembeni.
Akamwambia baba yake, "Inabidi nisimame, angalia hata magari makubwa yanaegesha pembeni na sioni vizuri mbele. Hali ni mbaya sana!" Baba yake akamwambia, "Usikate tamaa, wewe endelea kuendesha!" Tufani sasa ilizidi, lakini yule binti hakusimama na mara akaanza kuona japo kwa shida kidogo mbele yake. Baada ya maili kadhaa akajikuta yuko kwenye ardhi kavu ambako hakukuwa na mvua, na jua lilikuwa linaangaza.
Baba yake akamwambia, "Sasa unaweza kusimama na toka nje." Binti akauliza "Kwanini sasa?" Baba yake akamwambia "Ukitoka nje, tazama nyuma ili kuangalia watu waliokata tamaa na bado wako katikati ya tufani, kwa sababu hukukata tamaa tufani yako imekwisha sasa."
Huu ni ushuhuda wa kila mmoja wetu ambaye anapitia kwenye
Siyo kwa sababu kila mmoja, pamoja na wenye nguvu, wanakata tamaa haimaanishi hata wewe pia ukate tamaa. Kama utaendelea kupambana na kusonga mbele dhoruba yako itakwisha na jua litakuangazia nuru yake usoni kwako tena.
Kuna wengi wamekata tamaa na maisha na kujiona hawawezi tena kutoka, nikuhakikishie kuwa inawezekana kutoka hapo ulipo, unachotakiwa kufanya ni kimoja tu, simama tena na endelea mbele zaidi. Tuisikilize Sauti ya Mungu nasi tutayavuka majaribu japo yawe magumu kiasi gani.
Hadithi hii imenigusa na niaamini hata wewe imekugusa! Tafadhali nicheck kwenye 0785076937 au 0652211067 nikusaidie kupata kile kitu ambacho kimewasaidia wengi katika maisha na wengine hawakuwa na kitu kabisa na walikuwa wamekata tamaa kabisa ya maisha.
2017Shining_Year
Look_Great_and_Feel_Great
Its_Time_To_Shine_With_Oriflame
Make_Money
Have_Fun
Make_your_dream_reality
Be_Unstoppable
No comments:
Post a Comment