Sunday, September 16, 2018

Uthubutu

Tabia ya binadamu ni kuchukia mazingira yoyote mabaya yanayomzunguka. Na kimsingi hakuna anayependa mazingira mabovu/mabaya, huu ndiyo ukweli

Mbaya kuliko huwa tunapenda mteremko katika mambo mengi, hii ni kwa sababu ukitaka kufanya mabadiliko, ya vitu vingi gharama yake huwa kubwa kiasi cha kuwafanya wengi waogope kuchukua hatua.

Ukweli ni kwamba kile kitu kinachoogopwa na wengi, ndiyo chenye manufaa zaidi kuliko kile wengi wanachokimbilia. Na hii ndiyo sababu wanaofanikiwa ni wachache kuliko walioshindwa.

Kuna sababu kadha wa kadha zinazowafanya watu waogope kufanya mambo ya tofauti na wengine katika maisha lakini bado hali ya maisha waliyonayo hawaipendi, kubwa ikiwa ni gharama za kufanya mabadiliko/hatua ya kuondoka.

Wewe siyo mti, mahala/hali usipopenda/usiyoipenda haita kupeleka kwenye maisha ya ndoto zako, kuwa jasiri, anza kupiga hatua mpya na uone matunda leo.

#NsajigwaMwakigonja
#UnstoppableMan
#TeamUnstoppable
#Project1000
#TimeToEmpowerMorePeople

No comments:

Post a Comment