UNAWEZA"..
Siku chache zilizopita nikiwa napitia maandiko kadhaa katika mitandao ya kijamii nilikutana na andiko moja ambalo lilinitia moyo sana na hili ndilo nitakushirikisha..
Mwandishi wa lile andiko alikuwa akitoa salaam zake kwa msiba wa aliyekuwa mchezaji wa Yanga na Taifa stars. Mwandishi yule bila shaka alikuwa anamfahamu yule mchezaji tangu akiwa bado hajacheza ligi ngazi kuu ya taifa na timu ya taifa " taifa stars".
Mchezaji yule bila shaka alisoma shule mojawapo mkoani mbeya Tukuyu Secondary.
Kisa chake anakieleza kama ifuatavyo, "sitasahau siku ile tulipokuwa tumefungwa magoli sita kwa sifuri na wapinzani wetu, wewe ulipoingia ulisawazisha magoli yote na ukaongeza magoli mengine mawili tukatoka na Ushindi wa magoli nane kwa sita. Siku hii si tu alibadirisha matokeo ya mchezo ila alibadirisha hali ya wachezaji wenzake na washabiki. Na anasisitiza Yale magoli yote yalifungwa na wewe.
Inanifanya nikumbuke kile kisa cha mmiliki wa KFC ambaye alistaafu akiwa hajui nini atafanya lakini akiwa na hakika ya umaskini uliokuwa ukimsubiri. Lakini badaye alifanya self analysis " uchambuzi wa uwezo wake" na aligundua jambo moja alilokuwa anaweza kulifanya vizuri zaidi ambalo lilikuwa ni kutengeneza chicken (kuku)aliyeandaliwa kwa ajili ya kuliwa na yeye aliamua kutia bidii hivi Leo tunapozungumzia KFC ni biashara ya kimataifa na alikufa akiwa bilionea... Huyu alibadirisha matokeo....
Yule mwingine anaitwa Od Mandino msemaji na mwandishi mashuhuri wa kimarekani. Baada ya kutoka kupigana vita ya kwanza ya dunia alirudi nyumbani na aliamua kufanya kazi ya kuuza Bima lakini maisha yalikuwa magumu na akiwa amefilisika hakujuwa afanye nini badala yake akawa mlezi wa kupindukia. Siku moja akiwa njiani kurudi nyumbani aliona tangazo la bunduki iliyokuwa inauzwa kwa dola 29 na yeye mfukoni alikuwa na dola 30 tu "alifikiri kama nikinunua bunduki nitabakiwa na dola 1 inayotosha kununua risasi na nitaweza kujiua ili niepuke fadhaa hii....lakini haikutokea kabla ya kuamua aliona mbele kulikuwa na maktaba na alivutiwa kuingia na kusoma,badaye aliazimia kuwa na ratiba za Mara kwa Mara kwenda hapo na kusoma. Siku moja alikutana na kitabu kilichokuwa kimeandikwa na Napoleon na Clement, kilichokuwa kinazungumzia namna jinsi unaweza kufanikiwa....
Baada ya kusoma kile kitabu alidhamiria kwenda kufanya kazi ya kuuza Bima chini ya MTU mwingine na Mara alianza kuuza kwa mafanikio na baada ya muda aliandika kitabu cha kwanza ambacho kiliuza zaidi ya nakala 10,000,000 kilikuwa kimetafsiriwa zaidi ya lugha 5 duniani kwote.
Huyu pia aliweza kubadilisha matokeo....
Wewe pia unaweza!! Ukidhamiria kwa udhati na ukania kuthubutu na ukathubutu unaweza!!
Unaweza kubadilisha matokeo kuanzia Leo kama utakuwa unajua safari yako utokako, unakoenda na mbinu muhimu za kutanua, kuwa mwanafunzi wa wewe mwenyewe utapata kuwa mwalimu wa matokeo mazuri, daima usisumbue na historia yako ya utokako, bali anza kutafuta mabadiliko ya maisha yako leo.
Kuwa na Jumapili yenye mawazo chanya, yatakayo badilisa fikra zako milele.
Hakika unaweza na utafanikiwa zaidi ya vile ufikirivyo.
Karibu jiunge nami kubadilisha maisha yako leo kupitia Oriflame, Piga/SMS/WhatsApp 0785076937 au 0652211067 sasa.
No comments:
Post a Comment